Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________ 1 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA _____________ KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 (Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katiba ya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000. Dar es Salaam, A.J. CHENGE 1 Novemba, 2000 Mwanasheria Mkuu 2000 KIMEPIGWA CHAPA NA MPIGACHAPA WA SERIKALI DAR ES SALAAM - TANZANIA Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________ 2 KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 ____________ YALIYOMO _____________ Ibara Kichwa cha Habari UTANGULIZI SURA YA KWANZA JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA SEHEMU YA KWANZA JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU 1. Kutangaza Jamhuri ya Muungano. 2. Eneo la Jamhuri ya Muunga...